Rais Chakwera ahudhuria mazishi ya makamu Rais wake Chilima

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Lazurus Chakwera wa Malawi anawaongoza mamia ya maelfu ya waombolezaji wanaohudhuria mazishi ya makamu wake Saulos Chilima nyumbani kwake Ntcheu .

Marehemu Chilima aliye na umri wa miaka 51,alifariki kwenye ajali ya ndege ya kijeshi wiki iliyopita akielekea Khata Bay kwa mazishi ya Waziri mmoja wa zamani.

Rais Chakwera pia aliongoza makumi ya maelfu kuutazama mwili wa marehemu siku ya Jumapili, katika uwanja wa kitaifa wa Bingu mjini Lilongwe.

Chakwera aliahidi kufanywa uchunguzi wa kina kwa usadidi wa wataalam wa kutoka nje ya nchi kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *