Tembo wa Ivory Coast wamcharanga chui na kujaa fainali ya AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji Ivory Coast almaarufu The Elephants,  walijikatia tiketi kwa fainali ya makala ya  34 ya dimba la AFCON  baada ya kuwaangusha Chui wa Congo DR bao moja kwa bila katika nusu fainali ya Jumatano. 

Sébastien Hauller aliunganisha pasi ya Max Gradel na kuwanyanyua mashabiki wa nyumbani kwa goli la uongozi la dakika ya 65.

Licha ya kujaribu kila mbinu, chui walishindwa kurejea mchezoni na kuwapa tembo fursa ya kuandikisha historia kucheza fainali ya Jumapili dhidi ya Nigeria.

Ivory Coast wataangazia kuwa waandalizi wa kwanza kutwaa kombe hilo tangu mwaka 2006 Misri walipolinyakua.

Share This Article