Tebogo na Hassan watawazwa wanariadha bora wa mwaka

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Olimpiki Letsile Tebogo wa Botswana na Siffan Hassan wa Uholanzi, ndio washindi wa tuzo za wanariadha bora wa mwaka huu kwa wanaume na wanawake mtawalia.

Wawili hao walituzwa kwenye hafla iliyaondaliwa jana usiku mjini Monaco Ufaransa.

Tebogo alishinda dahahabu ya Olimpiki katika mita 200 akitumia sekunde 19.46 ,ikiwa rekodi ya Afrika akiangia kwenye kumbukumbu kuwa mwanariadha wa kwanza kutoka Botswana kushinda medali ya Olimpiki.

Hassan kwa upande wake alishinda dhahabu ya Olimpiki katika marathon,na shaba katika mita 5,000 na 10,000.

Tebogo pia alituzwa mwanariadha bora wa mbio za uwanjani, huku Hassan akipokea tuzo ya mwanariadha bora wa mashindano ya barabarani.

Sydney McLaughlin-Levrone wa Marekani alitawazwa mwanariadha bora wa mbio za uwanjani kwa wanawake wakati Mondo Duplantis wa Uswidi, akiibuka bora katika mashindano ya uwanjani naye Tamirat Tola wa Ethiopia akashinda tuzo ya mwanariadha bora wa mbio za barabarani kwa wanaume.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *