TD Jakes afichua kwamba alifanyiwa upasuaji wa dharura

Jumapili Novemba 24, 2024 Jakes alizirai alipokuwa akiendelea kuhubiri kwenye madhabahu na baadaye kanisa lake likatoa taarifa kwamba lilikuwa tatizo dogo la kiafya

Marion Bosire
1 Min Read

Askofu T.D. Jakes wa Marekani amefichua kwamba alifanyiwa upasuaji kama hatua ya dharura ya kuokoa maisha yake baada ya kuzirai kanisani wiki iliyopita.

Ametaja kupona kwake kuwa muujiza akisema alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi alipofikishwa hospitalini na ikagundulika kwamba alihitaji upasuaji huo haraka.

Jakes alihutubia washiriki wa kanisa lake la The Potter’s House, jana Jumapili kwa njia ya video ambapo wote walimwonyesha heshima kwa kusimama.

Askofu huyo hata hivyo hakufafanua anachougua lakini alisema anajibidiisha kurejelea hali yake ya kawaida huku madaktari wakimshauri apate mapumziko kwa wingi.

Alimalizia mahubiri yake mafupi kwa kauli kwamba watu wanaojitolea sana kulinda wengine kama yeye wanafaa kukumbuka kujijali pia.

Jumapili Novemba 24, 2024 Jakes alizirai alipokuwa akiendelea kuhubiri kwenye madhabahu na baadaye kanisa lake likatoa taarifa kwamba lilikuwa tatizo dogo la kiafya.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *