Tarehe ya Diddy kuondoka gerezani yabadilishwa tena

Marion Bosire
1 Min Read
P Diddy

Tarehe ya mwanamuziki wa Marekani Sean “Diddy” Combs kumaliza kifungo chake na kuondoka gerezani imebadilishwa kwa mara nyingine tena.

Diddy anayehudumia kifungo cha miezi 50 gerezani kutokana na mashtaka yanayohusiana na ukahaba atatoka kizuizini Aprili 25, 2028, kulingana na stakabadhi za usimamizi wa magereza Marekani.

Wakati wa kuhukumiwa kifungo mwaka jana, Combs aliwekewa Mei 8, 2028 kuwa tarehe ya kuondoka gerezani lakini baadaye ikabadilishwa hadi Juni 4, 2028.

Baba huyo wa watoto saba yuko katika gereza la Fort Dix huko New Jersey, alikopelekwa kutoka gereza la Metropolitan la New York Oktoba mwaka jana.

Viongozi wa mashtaka walikuwa wameiomba mahakama imhukumu Diddy kifungo cha miaka 11 gerezani wakisema kifungo cha muda mrefu kingempa muda wa kufikiria makovu ya kisaikolojia na ya kimwili aliyosababishia waathiriwa wake.

Hata hivyo mahakama iliamua kumpa muda wa miezi 50 gerezani.

Share This Article