Tanzania yafuzu kwa AFCON mwaka 2024 kwa mara ya tatu

Dismas Otuke
1 Min Read
230907F_ACNQ_ALGTNZ_DL

Tanzania wamefuzu kwa fainali za kombe la bara Afrika mwaka ujao nchini Ivory Coast, baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Algeria ugenini katika mechi ya kundi F,Alhamisi usiku mjini Annaba.

Taifa Stars wanafuzu kushiriki kipute hicho
cha Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019 nchini Misri waliposhinda mchuano mmoja na mara ya tatu kwa jumla huku wakiwa waakilishi pekee wa ukanda wa Afrika mashariki kwenye kipute cha mwakani.

Uganda walikosa kufuzu kutoka kundi hilo licha kusajili ushindi wa mabao mawili kwa bila ugenini dhidi ya Niger.

Share This Article