Wizara ya Afya nchini Tanzania imetuma kundi la wataalamu katika mkoa wa Kagera kuchunguza iwapo kuna maambukizi ya virusi vya Marburg.
Hii ni baada ya wizara hiyo kupokea tetesi za uwepo wa ugonjwa huo wa Marburg mkoani humo na sasa wataalamu hao watakusanya sampuli na kufanya vipimo vya maabara.
Waziri wa Afya wa Tanzania Jenista J. Mhagama amesema kufikia leo Januari 15, 2025, hakuna kisa kilichothibitishwa cha ugonjwa wa Marburg kutokana na sampuli zote zilizopimwa.
Mgahama anahakikishia wananchi na jamii ya kimataifa likiwemo Shirika la Afya Duniani – WHO kwamba wizara ya Afya imeimarisha mifumo ya kufuatilia magonjwa na itaendelea kutoa taarifa zaidi.
Virusi ya Marburg ni virusi vya homa ya kutokwa na damu na vinaweza kuambukiwa kupitia kutagusana na aina fulani ya mnyama popo au kutagusana na mtu aliyeambukizwa kwa kugusa unyenyevunyevu wa mwili au kujamiana.
Ugonjwa huo uliathiri mataifa ya Tanzania na Equatorial Guinea mwaka 2023 na mwaka 2024 taifa la Rwanda liliripoti chamuko la ugonjwa huo.