Tanzania kuwarejesha nyumbani raia wake 669 kutoka Afrika Kusini

Ubalozi wa Tanzania mjini Pretoria umetangaza kuwa utawahamisha raia wake kwa awamu  kuanzia Jumatano ijayo Agosti 26.

Dismas Otuke
1 Min Read

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekamilisha mipango ya kuwarejesha nyumbani raia wake walio nchini Afrika Kusini.

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka raia wake wote kurejea nyumbani na kujiunga na familia zao  baada ya kuishi Afrika Kusini kwa kipindi kirefu.

Ubalozi wa Tanzania mjini Pretoria umetangaza kuwa utawahamisha raia wake kwa awamu  kuanzia Jumatano ijayo Agosti 26.

Kundi la kwanza litawajumuisha wa Watanzania 241 walio mkoani Kwazulu Natal.

Raia 669 wa Tanzania wanaishi nchini Afrika na wanatarajiwa kurejeshwa nyumbani.

Mpango huo utatanguliwa na zoezi la kuwatathmini raia halisi litakaloandaliwa mapema juma lijalo.

Share This Article