Msomi wa kiisilamu ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir alitangaza jana kwamba mwezi ulionekana katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania na katika nchi jirani.
Kutokana na hilo, Sheikh Abubakar Zubeir alisema kwamba maadhimisho ya Eid Al Fitri ni leo Jumatatu Machi 31,2025.
Kiongozi huyo wa dini alitoa tangazo hilo akiwa jijini Dar es salaam ambapo alisema, “Nawatangazia Waislamu wote kuwa mwezi umeandama na umeonekana na kushuhudiwa sehemu nyingi katika nchi yetu, pia umeonekana Kenya, Pemba na Arusha”.
Aliendelea kusema kwamba wengi wliuona mwezi hio waziwazi na yeye akauthibitisha na hivyo leo ndio Eid nchini Tanzania.
Haya yanajiri baada ya waisilamu nchini Kenya na Uganda kuadhimisha Eid jana Jumapili Machi 30, 2025.
Kupishana kwa siku hiyo ya maadhimisho ya Eid ni jambo ambalo huwa linashuhudiwa mara kwa mara kote ulimwengini na hivyo hapajaharibika jambo.
Hata hivyo serikali nchini Kenya ilitenga leo Jumatatu kuwa maadhimisho ya kitaifa ya Eid Al Fitri.