Takwimu za AFCON baada ya mechi 50 huku kilele ikiwa Jumapili

Dismas Otuke
1 Min Read

Mechi 50 zimesakatwa tangu kuanza kwa makala ya 34 ya kipute cha kombe la AFCON nchini Ivory Coast.

Jumla ya ambao 116 yamefungwa kutokana na mechi 50,Emilio Nsue wa Equitorial Guinea akiongoza chati ya ufungaji mabao kwa magoli matano,moja zaidi ya Gelson Dala wa Angola na Mostafa Mohammed wa Misri.

Kumekuwa na mabao manne ya kujifunga katika kindumbwendumbwe hicho .

Kati ya timu 24 zilizoanza mashindano hayo,tayari timu 20 zimeyaaga mashindano huku nne pekee zikisalia.

DR Congo wameratibiwa kumenyana na Bafana Bafana ya Afrika Kusini katika mchuano wa kuwania nafasi ya tatu na nne siku ya Jumamosi, kabla ya wenyeji Ivory Coast kuwatumbuiza Nigeria katika pambano la fainali Jumapili usiku.

Ili kufuzu kwa fainali Ivory Coast iliwashinda DR Congo bao moja kwa bila huku Nigeria ikiwalemea Afrika Kusini kupitia mikiki ya penati katika hatua ya nusu fainali.

Nigeria na Ivory Coast watakuwa wakichuana kwa mara ya pili baada ya Super Eagles kuwashinda tembo wa Ivory Coast bao moja kwa bila katika mechi ya kundi A.

Share This Article