Jumla ya watoto 1,957,476 walio chini ya umri wa miaka mitano,walipokea chanj dhidi ya ugonjwa wa kupooza katika awamu ya kwanza iliyokamilika maajuzi ikiwa asilimia 104 nukta 2.
Awamu ya pili ya kutoa chanjo hii itangóa nanga Septemba 28 hadi Oktoba mbili kote nchini.
Kampeini ya chanjo ya Polio ilitekelezwa na wizara ya afya kama njia ya kuchukua tahadhari kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa kupooza katika kambi ya wakimbizi ya Hagadera kaunti ya Garissa.
Chanjo hiyo itolewa katika kaunti 10 wakati wa awamu ya kwanza iliyotekelezwa kati ya Agosti 24 na 28 mwaka huu .
Kaunti zilizolengwa katika amamu ya kwanza zilikuwa Kiambu, Nairobi, Kajiado na Garrissa huku awamu ya pili inayotarajiwa mwezi ujao ikifanyika katika kaunti za Kiambu, Nairobi, Kajiado, Garrissa, Kitui, Machakos, Tana River, Lamu, Wajir na Mandera.