Takamoto ashinda mbio za WRC Safari rally

Dismas Otuke
1 Min Read

Katsuta Takamoto wa kampuni ya magari ya Toyota Gazoo ndiye bingwa mpya wa mashindano ya magari ya WRC Safari Rally yaliyokamilika Jumapili mjini Naivasha.

Takamoto alimaliza sekunde 27.4 mbele ya Adrien Fourmax, aliyechukua nafasi ya pili huku Sami Pajari pia wa Toyota Gazoo akiambulia nafasi ya tatu.

Ulikuwa ushindi wa kwanza wa Takamoto mwenye umri wa miaka 33, baada ya kumaliza wa pili mwaka jana.

Karan Patel alimaliza wa saba katika kitengo cha WRC 2.

Elfyn Evans baada ya mikondo mitatu anaongoza msimamo kwa alama 66, akifuatwa na Solberg kwa pointi 58 huku Takamoto akishikilia nafasi ya tatu kwa pointi 55.

Share This Article