AFCON: Taifa Stars kumenyana na Atlas Lions Jumatano usiku

Tom Mathinji
1 Min Read
Timu ya Taifa Stars ya Tanzania.

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania almaarufu Taifa Stars leo Jumatano itakabiliana na Morocco katika kipute cha AFCON katika mchuano utakaosakatwa katika uwanja wa Laurent Pokou, San Pedro saa mbili usiku.

Taifa Stars inakabiliwa na kibarua kigumu inapojiandaa kumenyana na timu ambayo imeorodheshwa ya kwanza barani Afrika, na iliyoandikisha historia kwa kuwa timu ya kwanza Afrika kufuzu kwa nusu fainali za kombe la dunia mwaka 2022.

Aidha, timu hiyo ya Afrika Mashariki inaingia katika mechi hiyo huku ikijivunia safu ya ulinzi ambayo ilijizatiti kuhakikisha nyavu zake hazitikiswi wakati wa mechi za kufuzu kwa kipute hicho.

Taifa stars na Morocco ziko katika kundi F, pamoja na Zambia na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Timu hizo mbili zimekutana mara tano ambapo Taifa Stars imeishinda Morocco mara moja na kushindwa mara nne na Atlas Lions.

Mechi hiyo itaonyeshwa mubashara na runinga ya KBC Channel 1.

Share This Article