Super Eagles ya Nigeria waliendeleza ubabe dhidi ya Indomitable Lions wa Cameroon, baada ya kuwazabua mabao mawili kwa nunge na kutinga robi fainali ya AFCON.
Ademola Lookman alifunga magoli yote moja katika kila kipindi, na kuifuzisha Nigeria kwa awamu ya nane bora.
Cameroon waliyaaga mashindano katika raundi ya 16 bora kwa mara pili mtawalia.
Nigeria watakumbana na Angola katika robo fainali wiki ijayo.