Taharuki yatanda DRC baada ya uchaguzi mkuu

Dismas Otuke
1 Min Read

Hali taharauki imezidi kutanda katika Jamhuri ya Demorasia ya Congo  takriban siku kumi tangu kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu.

Tume huru ya uchaguzi CENI siku ya Alhamisi wiki hii ilimtangaza Rais Felix Tshisekedi kuwa mshindi wa kwa kupata asilimia 80 ya kura zilizopigwa.

Kumekuwa na makabiliano makali kati ya polisi na wafuasi wa upinzani wanaopinga matokeo ya kura za Urais wakitaka kurejelewa kwa zoezi hilo kwa madai ya wizi wa kura.

Waangalizi wa kimataifa pia wametilia shaka uhuru na uwazi wa uchaguzi huo, lakini serikali imesimama kidete kufutilia mbali uwezekano wa marudio ya uchaguzi.

Share This Article