Sururu ateuliwa kuwania tuzo bora ya SOYA kwa walemavu

Dismas Otuke
1 Min Read

Mpigaji makasia Asiya Sururu,ameteuliwa kuwania tuzo ya mwanamichezo bora mlemavu wa mwaka katika tuzo za kila mwaka za SOYA.

Asiya ambaye anashikilia rekodi mbili za dunia, pia alivunja rekodi ya dunia katika mashindano ya Concept 2 ya muda wa dakika 60 kwa umbali wa mita 11,243 Oktoba 7 mwaka
uliopita.

Sururu,ameteuliwa kuwnania tuzo huyo pamoja na mchezaji tennis Purity Jepkirui Kandie, Nancy Chelangat na Ruth Chemurgor  .

Mshindi atatangazwa wakati wa hafla ya 20 ya tuzo za SOYA zitakazoandaliwa tarehe 23 mwezi huu katika kaunti ya Nairobi.

Share This Article