Tume ya kushughulikia mishahara na marupurupu nchini SRC, imetetea pendekezo lake la kuongeza mishahara ya wafanyikazi wa ngazi za juu wa serikali huku ikisema kuwa mapendekezo hayo yalipaswa kutekelezwa mapema na lakini yakaathiriwa na janga la Covid-19.
Akiwahutubia wanahabari Jumamosi, mwenyekiti wa tume hiyo Lynn Mengich alisema kuwa pendekezo hilo lilikuwa tu sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya awali ya nyongeza ya mishahara.
Siku ya Ijumaa, Rais Wiiliam Ruto alitangaza nyongeza ya mishahara ya kati ya asilimia saba na kumi kwa wafanyikazi wa serikali kuanzia mwezi huu wa Julai.
Alidokeza kuwa mpango wa nyongeza ya mishahara ulisitishwa kutokana na janga la Covid-19, na kwamba pendekezo la hilo lililenga kuziba pengo lililosababishwa na Covid 19 pandemic.
Juma hili kupitia arifa, tume ya SRC ilipendekeza nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa wakuu wa serikali kwa asilimia 14, ili kuwakinga dhidi ya hali ngumu ya kiuchumi inayoshuhudiwa Kwa sasa
Hata hivyo, Rais William Ruto alipinga nyongeza hiyo na badala yake akapendekeza nyongeza ya mshahara ya kati ya asilimia saba na kumi kwa watumishi wote wa umma kuanzia mwezi huu wa Julai.