Spika wa bunge la taifa Moses Wetang’ula aliwasili nchini Djibouti jana jioni kwa ziara rasmi ya siku mbili.
Ziara hiyo inaangazia uimarishaji wa uhusiano mwema kati ya Kenya na Djibouti.
Alilakiwa na Rais wa bunge la taifa nchini Djibouti Dileita Mohamed Dileita.
Spika Wetang’ula anatarajiwa kuhutubia bunge la taifa hilo leo.
Ameandama na wabunge Jane Kagiri ambaye ni mwakilishi wa kaunti ya Laikipia, Zaheer Jhanda wa eneo bunge la Nyaribari Chache na Mohammed Adan Daud wa eneo bunge la Wajir Mashariki.