Spika Wetang’ula awaasa wabunge wanaosimamia kamati

Dismas Otuke
1 Min Read

Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula amewaonya wenyeviti wa kamati za bunge wanaokosa vikao kuwa watapokonywa nafasi zao iwapo wataendelea kususia vikao hivyo.

Akiwatubia wabunge wakati wa mkutano wa siku tatu unaofanyika mjini Niavasha, Wetang’ula amesema ipo haja ya kulainisha shughuli za bunge ili kutochelewesha kufanyika kwa vikao.

Amewaonya wenyeviti wa kamati za bunge wanaoendelea kukosa vikao kuwa nafasi zao zitakabidhiwa manaibu wao.

Ameongeza kuwa misuada yoyote ambayo wawasilishi wake hawatakuwepo bungeni wakati wa kutajwa kwake itatupiliwa mbali.

Website |  + posts
Share This Article