Sonko na wenzake waondolewa lawama kwenye kesi ya ufisadi

Marion Bosire
1 Min Read

Gavana wa zamani wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko na wengine 16 wameondolewa lawama kwenye kesi ya ufisadi wa shilingi milioni 357 kufuatia kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

Hakimu Eunice Nyutu katika uamuzi wake wa leo alisema kwamba hakuna ushahidi uliowekwa mbele ya mahakama unaotosha kushtaki watu hao kwa kosa la ufisadi.

Kulingana naye upande wa mashtaka ulisambaratisha kesi hiyo baada ya kufikisha mashahidi 6 pekee mahakamani ilhali ulikuwa umeashiria kwamba una mashahidi 38.

Washtakiwa wote 19 wa kesi hiyo walikuwa wameshtakiwa kwa makosa 19 ya ufisadi kila mmoja.

Wanadaiwa kushirikiana kufuja pesa za umma shilingi 357,390,299.95 skutoka kwa serikali ya kaunti ya Nairobi kati ya Mei 24, 2018 na Machi 8, 2019.

Walishtakiwa pia kwa makosa ya kujipatia pesa kwa njia isiyo halalli na kupokea pesa zilizotokana na uhalifu.

Hata hivyo mahakama ilisema kwamba hakukuwa na ushahidi wa kudhihirisha kwamba walitekeleza makosa hayo.

Share This Article