Somalia imejumuishwa rasmi katika jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano viongozi wa Afrika Mashariki, ulioandaliwa Jijini Arush Tanzania.
Taifa hilo sasa linajiunga na Kenya, Burundi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda na Tanzania.
Hatua hiyo ilifuatia uamuzi wa mkutano wa kawaida wa 23 viongozi wa Afrika Mashariki, ulioandaliwa mjini Arusha Tanzania.
Kujumuisshwa kwa Somalia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, kunatokana na majadiliano yaliyoagizwa na mkutano wa 22 wa viongozi wa Afrika Mashariki.
Kuingia kwa Somali katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, kunatarajiwa kutabuni fursa zaidi za kibiasharana utangamano katika kanda hiyo.
Somalia pia itaimarisha rasilimali za uchumi wa baharini katika mataiafa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano huo uliandaliwa baada ya kukamilika kwa ule uliojadili mabadiliko ya tabia nchi na usalama wa chakula, pia ulishuhudia kuchaguliwa kwa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kuwa mwenyekiti wa mkutano wa viongozi wa mataifa ya Afrika Mashariki.
Kiir anachukua wadhifa huo kutoka kwa mwenzake wa Burundi Évariste Ndayishimiye ambaye muhula wake unakamilika.