Slovakia kuipa Kenya usaidizi wa kiufundi kuimarisha usalama wa chakula

Tom Mathinji
1 Min Read

Serikali ya Slovakia itatoa usaidizi wa kiufundi kwa Kenya, ili kupiga jeki uwezo wa taifa hili kujitosheleza kwa chakula.

Balozi wa Slovakia hapa nchini Katarina Leligdonova, alisema taifa hilo linadhamini uhusiano uliopo kati nchi hizo mbili, na liko tayari kutoa utaalam wake katika nyanja  mbali mbali hususan kuhusu vyakula vinavyotoa protini, ili kuwasaidia walio na mahitaji.

Balozi huyo aliyekuwa akiongoza ujumbe wa maafisa wa serikali ya Slovakia katika ziara ya miradi kadhaa  nchini Kenya, alisema nchi yake itatoa msaada kwa raia wa Kenya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

“Tunataka kuwa na mjadala kuhusu maswala ya mazingira na usalama wa chakula. Miradi inayotolewa na Slovakia, ni kuhusu kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga,” alisema alipozuru kituo cha wadudu kilichoko Limuru, Kaunti ya Kiambu, ambacho huwafuga wadudu wanaotumiwa kama chanzo mbadala cha protini.

Kituo hicho ni nyumbani kwa aina tatu ya wadudu. Wadudu aina ya Crickets na  millworms hufugwa kutoa virutubishi kwa binadamu, huku wadudu aina ya  mill worms, wakisambaziwa wakulima wadogo wadogo kote nchini

TAGGED:
Share This Article