Mabingwa watetezi Senegal ndiyo timu ya pili kutinga raundi ya pili ya kindumbwendumbwe cha AFCON, baada ya kuwakalifisha Cameroon mabao matatu kwa moja katika mechi ya kundi C Ijumaa jioni.
Simba wa Teranga walianza mechi vizuri huku wakichukua uongozi kunako dakika ya 16 kupitia kwa Ismaila Sarr kabla ya kumdokolea Habbib Diallo, pasi naye akatanua uongozi kipindi cha pili dakika ya 71.
Jean-Charles Castelletto alikomboa bao moja kabla ya Sadio Mane kuhitimisha shughuli kwa goli la tatu.
Kufuatia ushindi huo Senegal wamejihakikishai nafasi ya kwanza kundini C kwa pointi 6 wakisalia na mchuano wa mwisho dhidi ya Guinea.
Cameroon itawalazimu kuwashinda Gambia kwa idadi kubwa ya magoli, ili kuwa na fursa ya kufuzu kwa raundi ya pili.