Wenyeji Cameroon wameititiga Kenya mabao 4-1 katika mchuano wa kundi J,kufuzu AFCON mwaka ujao uliosakatwa ugani Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde Ijumaa jioni.
Simba wa Indomitable walifungua karamu ya magoli kunako dakika ya nane kupitia kwa nahodha Vincent Aboubakar aliyeunganisha tuta na penati.
Martin Hongla na Brayan Mbeumo waliongeza moja kila mmoja kwa wenyeji huku nahodha Michael Olunga,akikomboa moja na kipindi cha kwanza kumalizika kwa uongozi wa 3-1 kwa faida ya Cameroon.
Christian Basongog alibusu nyavu mwanzoni mwa kipindi cha pili huku wenyeji wakipata ushindi mkubwa na kuongoza kundi J kwa pointi 7 .
Timu hizo zitakumbana tena Jumatatu ijayo jijini Kampala Uganda .
Indomitable Lions wamechupa kileleni kwa alama 7,wakifuatwa na Zimbabwe kwa pointi 5 ,moja zaidi ya Kenya iliyo ya tatu.
Cameroon wanahitaji ushindi dhidi ya Kenya Oktoba 14, ili kufuzu kwa fainali za AFCON zitakazoandaliwa nchini Morocco kati ya Disemba mwaka ujao na Januari mwaka 2026