Miamba wa soka Tanzania bara, kilabu ya Simba, walifuzu kwa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kuishinda Al Masry ya Misri katika duru ya pili ya kwota fainali jana jioni katika mji wa Dares Salaam.
Wekundu ya Msimbazi iliyokuwa imeshindwa mkumbo wa kwanza magoli 2-0 jijini Cairo, iliwasinda wageni hao pia mbili bila, Elly Mpanzu na Stephen Mukwala wakifunga magoli hayo kunako kipindi cha kwanza.
Katika awamu ya matuta Simba walifunga penati nne huku Masry, wakifunga mkwaju mmoja tu.
Ni mara ya kwanza kwa Simba kufuzu kwa nusu fainali ya Kombe la Afrika baada ya kubanduliwa katika rob0 fainali ya Ligi ya mabingwa mara mbili.