Shule zote za msingi na za upili za umma zimefunguliwa kufikia mwisho wa Jumatano, Januari 8 kwa muhula wa kwanza, ila huenda shughuli za masomo zikatatizika pakubwa kutokana na serikali kuchelewa kutoa pesa.
Serikali inapaswa kutoa asilimia 50 ya fedha kugharimia masomo kwa shule za msingi na zile za upili za umma.
Hata hivyo, kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara ya Elimu, serikali bado haijapata pesa hizo.
Kando na usambazaji unaosuasua wa vitabu vya kiada, shughuli nyingine muhimu za masomo huenda zikalemazwa kutokana na ukosefu wa fedha.
Hazina Kuu inapaswa kutoa shilingi bilioni 48 kugharimia shughuli za masomo kwa muhula huu ambazo haziko tayari kwa sasa.
Muhula huu wa kwanza una jumla ya majuma 13 .