Shule za Kisii na Kinale zavuna ushindi kwenye mashindano ya kitaifa

radiotaifa
1 Min Read

Shule za Kisii, Kinale, Upper hill, na St.Mary’s Yala, zimevuna ushindi wa kwanza wa mechi za kwanza za makundi katika mashindano ya kitaifa ya muhula wa kwanza ya raga ya wachezaji 15 kila upande baina ya shule za upili yanayoendelea Jijini kisumu.

Kwenye michuano hiyo, Kisii iliishinda Kakamega alam 16 kwa 14, Upper hill ikailaza Kwale High alama 26 kwa sufuri, Menengai ikaipiku Mang’u alama 46 kwa tano, nao wenyeji Yala wakawalemea mabingwa wa mwaka juzi All St. Embu alama 10 kwa nane.

Kwenye kitengo cha vipusa kinale waliwaadhibu St.Joseph alama 22 kwa sufuri.

Katika handiboli ya warembo, Moi Girls Kamusinga waliwakwatua wenyeji Nyakach alama 27 kwa 19 wakati Kyeni wakiwaadhibu St.Claire alama 28 kwa 26.

Kwenye uga wa Magongo, wenyeji Kisumu walishindwa kuhimili makali ya wageni St.Antony walipozabwa bao moja kwa nunge shuleni mwao.

Siku ya Jumatano kila timu itasakata mchuano wa pili.

Taarifa na Boniface Musotsi.

Share This Article