Shule ya upili ya Cardinal Otunga yapokea matokeo ya KCSE

Tom Mathinji
1 Min Read
Shule ya upili ya Cardinal Otunga yapokea matokeo ya mtihani wa KCSE wa mwaka 2023.

Matokeo ya mtihani wa KCSE wa mwaka 2023 wa shule ya upili ya Cardinal Otunga yaliyokuwa yamezuiliwa, hatimaye yametolewa huku watahiniwa wote wakifuzu kujiunga na vyuo vikuu.

Baraza la mitihani hapa nchini KNEC, lilikuwa limezuilia matokeo ya mtihani wa KCSE ya wanafunzi 50 kati ya wanafunzi 433 waliofanya mtihani huo, kwa tuhuma za udanganyifu.

Watahiniwa sita walipata alama ya A , 60 wakapata alama ya A- huku wanafunzi 376 wakipata zaidi ya alama ya B-. Shule hiyo ilirekodi alama ya wastani ya 9.6.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Albert Obiro aliwapongeza watahiniwa hao na washikadau ikiwa ni pamoja na kanisa katoliki ambalo lilikuwa mdhamini, kwa ushirikiano wao uliohakikisha matokeo bora.

Shule kadhaa bado hazijapokea matokeo ya mtihani wa kidato cha nne KCSE wa mwaka jana.

Share This Article