Shule kufunguliwa kwa muhula wa kwanza Januari 6

Dismas Otuke
1 Min Read
Julius Ogamba, Waziri wa Elimu

Shule zote kote nchini zitafunguliwa rasmi kwa muhula wa kwanza Jumatatu ijayo, Januari 6.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara ya Elimu, muhula wa kwanza wa mwaka huu utakuwa na jumla ya wiki 13, zikiwemo siku 5 za mapumziko ya katikati ya muhula.

Mtaala mpya wa elimu ya umilisi, CBC utashuhudia wanafunzi wa kundi la kwanza wakijiunga na Gredi ya 9.

Aidha serikali imetangaza kukamilishwa kwa ujenzi wa madarasa 16,000 ya CBC uliogawanywa kwa awamu nne ukiwa katika  asilimia 93 kukamilika.

Pia ili kufanikusha mtaala wa CBC, Wizara ya Elimu imenunua vitabu vya kiada  9,926,618, ambavyo vitasambazwa kwa shule zote kote nchini.

Wizara hiyo pia imetenga  asilimia 50 ya fedha za kufadhili elimu kwa muhula wa kwanza, asilimia 30 katika muhula wa pili na asilimia 20 kwa muhula wa tatu.

 

 

 

 

 

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *