Shujaa yatua nchini na kulakiwa kibabe baada ya kurejea kwa mashindano ya Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande maarufu kama Shujaa, imerejea nyumbani mapema leo Alhamisi kutoka mjini Sao Paulo, Brazil, ilikofanikiwa kupandishwa ngazi kushiriki mashindano ya dunia ya HSBC.

Familia na marafiki walijiunga na wachezaji wa timu hiyo kusherehekea ufanisi huo.

Kenya ilimaliza ya pili katika msururu wa Brazil wa divisheni ya pili.

Shujaa imo kundi C katika mashindano ya  msururu wa Dunia ya Hong Kong Pamoja na Australia, New Zealand na Marekani huku mashindano  yakiandaliwa kati ya tarejhe 17 na 19 mwezi huu.

Share This Article