Shujaa yajumuishwa kundi C katika msururu wa Perth, Australia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande, maarufu kama Shujaa, imejumuishwa kundi C, katika msururu wa tatu wa Perth, Australia, utakaondaliwa kati ya Januari 24 na 26.

Kenya itafungua ratiba Januari 24 dhidi ya New Zealand kabla ya kukabiliana na viongozi wa msururu wa Fiji na kisha wamalize ratiba dhidi ya Uruguay Januari 25.

Shujaa ni ya tisa kwenye msimamo wa dunia kwa alama 11, baada ya kuzoa pointi 3, katika msururu wa Dubai na ikazoa alama 8 katika msururu wa pili wa Cape Town.

Timu hiyo imekuwa kambini kujiandaa kwa mashindano hayo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *