Shujaa yaibamiza Afrika Kusini msururu wa Dubai

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya raga kwa wanaume saba upande imeimarika na kusajili ushindi wa alama 22-17 dhidi ya Afrika Kusini, katika mechi ya pili ya kundi A ya a msururu wa kwanza wa Dubai Sevens.

Kevin Wekesa,Patrick Odongo Okong’o  na Tristan Leyds  wakafunga try moja, huku Nygel Pettersan Amaitsa akipachika try mbili naye Nygel Pettersan Amaitsa  akaunganisha conversion.

Afrika Kusini imejipatia tries zake kupitia kwa Tristan Leyds, aliyefunga mbili, naye Donavan Don akaongeza moja huku Tristan Leyds akifunga conversion.

Shujaa ilianza vibaya msururu huo mapema Jumamosi ilipoambulia kichapo cha alama 24-19  kutoka kwa  Ufaransa .

Kenya itarejea uwanjani kwa mchuano wa mwisho dhidi ya Australia Jumamosi jioni .

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *