Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande imetwaa ubingwa wa mshindano ya World Rugby Sevens Challenger baada ya kuipiku Chile alama 12-7 kwenye fainali iliyosakatwa katika uwanja wa Dubai Jumapili.
Patrick Odongo alifunga try moja kila kipindi huku Kenya wakiongoza kipindi cha kwanza kwa alama 7-5.