Shujaa kushiriki mashindano ya Singapore Sevens

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga kwa wachezaji saba kila upande iliyopandishwa ngazi jana, itashiriki mashindano ya msururu wa kwanza wa dunia ya Singapore, mapema mwakani.

Shujaa iliyoshushwa ngazi mwishoni mwa msimu  wa mwaka 2024 na 2025,  ilipandishwa huku ikishinda medali ya fedha latika msururu wa tatu na wa mwisho wa Sao Paulo,Brazlil.

Kenya ilimaliza ya pili kwa jumlaya pointi 50, kutokana na misururu hiyo mitatu ya divisheni ya pili.

Msururu wa Singapore utakuwa wa kwanza msimu wa mwaka 2027 ukiandaliwa kati ya Januari  31 na Februari mosi.

Share This Article