Shujaa kuondoka Jumatatu kwa Olimpiki

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Raga ya Kenya kwa wachezaji saba upande Shujaa, imeratibiwa kuondoka nchini Jumatatu ijayo Julai 8 kwa michezo ya Olimpiki .

Katibu Mkuu wa kamati ya Olimpiki nchini NOC-K Francis Mutuku, alisema haya Jumamosi mjini Naivasha, akihudhuria warsha ya siku mbili ya wanahabari wa michezo, iliyoandaliwa na shirika la kukabiliana dhidi ya ulaji muku- ADAK.

Mutuku amesema kuwa timu hiyo itapiga kambi ya wiki mjini Miramas, kabla ya kuelekea Paris kwa michezo ya Olimpiki makala ya 31.

Kikosi cha pili kusafiri kuelekea Ufaransa kitakuwa cha timu ya taifa ya Voliboli ya wanawake maarufu kama Malkia Strikers, siku mbili baadaye huku wanariadha wa mbio za masafa mafupi wakifuatia baadaye wiki ijayo.

Katibu huyo amesisitiza kuwa wanariadha wote watalipwa marupurupu yao kikamilifu, kabla ya kusafiriki kwa michezo hiyo.

Kenya itashiriki fani ya Raga wanaume,Voliboli wanawake,Kitwara,Uogeleaji,Riadha na Judo.

Makala ya 31 ya Olimpiki yataandaliwa kati ya Julai 26 na Agosti 11 mwaka huu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *