Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande – Shujaa, itashuka uwanjani Wanda Metropolitana kukabiliana na Ujerumani katika mechi ya kufuzu kushiriki mashindano ya msururu wa dunia, HSBC msimu ujao.
Kenya wanaofunzwa na Kevin Wambua walifungua mashindano hayo ya Madrid Sevens Ijumaa kwa ushindi wa pointi 19-12 dhidi ya Samoa, kabla ya kuangushwa alama 10-5 na Uhispania na hatimaye kuititiga Chile pointi 36-7 Jumamosi.
Kenya ilimaliza ya pili katika msimamo kwa alama 36 sawa na Uruguay.