Shujaa kukaza misuli Cape Town baada ya kutepetea Dubai

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Raga ya Kenya maarufu kama Shujaa itafungua msururu wa pili wa mashindano ya Dunia wa Cape Town Afrika Kusini dhidi ya Australia kesho.

Mechi hiyo ya kundi B itang’oa nanga saa sita adhuburi,kabla ya kumenyana na Uhispania saa tisa na robo .

Kenya iliyo na chipukizi wengi ilizoa pointi tatu katika msururu wa kwanza wiki jana.

Shujaainarejea katika mashi dano ya msururu baada ya kukosa msimu jana, baada ya kushushwa daraja mwaka 2022.

Ketika msururu huo kundi A linajumuisha mabingwa wa Dubai Fiji,Uingereza na Uruguay.

Kundi C lina Argentina,wenyeji Afrika Kusini na Ireland kisha, kundi D linajumuisha New Zealand,Ufaransa na Marekani.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *