Shujaa kujaribu bahati tena Singapore Sevens

Shujaa itafungua ratiba ya kundi B dhidi ya Ireland, kabla ya kufunga mechi za makundi dhidi ya Ufaransa kesho.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande -Shujaa, itarejea kwa msururu wa sita wa Singapore Sevens, baina ya kesho na Jumapili wakilenga kujinusuru dhidi ya kuenguliwa.

Shujaa itafungua ratiba ya kundi B dhidi ya Ireland, kabla ya kufunga mechi za makundi dhidi ya Ufaransa kesho.

Kenya ilizoa pointi tatu katika msururu wa wiki jana wa Hong Kong, ikiwa ya tisa katika msimamo wa dunia kwa alama 18  baada ya misururu 5.

Matokeo bora zaidi ya Kenya msimu huu yalikuwa kumaliza ya saba katika msururu wa pili ulioandaliwa Cape Town Afrika Kusini.

Website |  + posts
Share This Article