Shirikisho la Mpira wa Wavu Nchini lapongezwa

radiotaifa
1 Min Read
Wachezaji wa zamani wa mpira wa wavu wamepongeza hatua ya Shirikisho la Mpira wa Wavu Nchini kuelekeza mashindano ya mchezo huo mashinani. 
Wakizungumza kwenye fainali za Kombe la Mbunge wa Lugari Nabii Nabwera katika Uwanja wa Shule ya Msingi ya Maturu katika eneo bunge hilo, ambayo ilishirikisha timu zote nchini, wachezaji wa zamani Dorcas Nandasaba, Philip Mayo, na Benard Musumba wanasema itakuwa vyema kwa mchezo huo kuelekezwa mashinani.
Katibu wa Shirikisho la Mpira wa Wavu kaunti ya Kakamega, Osinde Wamusia, aliteua Mbunge wa Lugari Nabii Nabwera kuwa kinara wa mpira wa wavu katika eneo la Kakamega, akisema kuelekezwa kwa mchezo huo mashinani kutakuza talanta za vijana wengi.
Mbunge wa Lugari Nabii Nabwera, akisema atashirikiana na Shirikisho la Mpira wa Wavu kufufua mchezo huo eneo la Magharibi.
Taarifa ya Carolyn Necheza
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *