Shirika la reli larejelea uchukuzi wa abiria Jijini Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read
Huduma za uchukuzi wa reli zarejelewa Nairobi.

Shirika la reli nchini limetangaza kurejelewa kwa shughuli zake za uchukuzi katika baadhi ya maeneo Jijini Nairobi.

Kupitia kwa taarika katika mtandao wake wa X siku ya Jumatatu, shirika hilo lilisema huduma zake zimerejea katika maeneo ya Embakasi Village, Lukenya, reli inayoelekea katika kituo cha SGR na Syokimau kuanzia Jumanne

Hata hivyo, shirika hilo lilisema huduma katika maeneo ya Limuru na Ruiru bado zimesitishwa kutokana na shughuli ya ukarabati zinazoendelea kufuatia mvua kubwa.

“Hudumu za uchukuzi wa reli hubadilika mara kwa mara, kulingana na hali ya anga na maswala mengine ya kiusalama,” ilisema taarifa ya shirika hilo.

Juma lililopita, shirika la reli nchini lilisimamisha utoaji huduma za uchukuzi wa abiria kutoka Jijini Nairobi hadi katika maeneo mengine, kutokana mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa inayonyesha hapa nchini.

Share This Article