KLM yapokea tuzo ya APEX kwa mwaka wa tatu mtawalia

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirika la ndege la KLM limepokea tuzo ya APEX World Class Award kwa mwaka wa tatu mtawalia kutokana na utoaji huduma bora.

Tuzo hiyo hutolewa kila mwaka na chama cha kimataifa cha APEX, huku washindi wakibainika kupitia kwa ukaguzi unaofanywa kupitia kwa hisia za abiria kuhusu huduma zinazotolewa.

Mashirika manane ya ndege yalipokea tuzo za mwaka huu yakiwemo KLM, Emirates, Singapore Airlines, Qatar Airways, Japan Airlines, Xiamen Airlines na Saudia.

TAGGED:
Share This Article