Shirika la ndege Kenya Airways (KQ) na shirika la kimataifa kuhusu wahamiaji IOM, zimetia saini mkataba wa kukabili ulanguzi wa wanadamu na uhamiaji usio halali.
Shirika hilo linatarajiwa kutumia ushawishi wake kimataifa na sera mpya kuhusu ulanguzi wa wanadamu kuripoti visa vya ulanguzi wa binadamu.
Afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo Allan Kilavuka, alisema mkataba huo utasaidia utekelezwaji wa hatua za kutambua, kuzuia na kukabili ulanguzi wa watu.
Barani Afrika, Kenya ni taifa ambalo hutumika pakubwa kwa shughuli haramu ya ulanguzi wa binadamu.
Shirika la IOM limesema Kenya hunakili zaidi ya wahamiaji milioni moja wa kimataifa, na zaidi ya watu nusu milioni wanaotafuta uhamisho au wakimbizi.