Watu 24 wameripotiwa kufariki katika shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lilitokea kwenye gari mjini Quetta nchini Pakistan siku ya Jumapili.
Watu wengine 50 walijeruhiwa huku kundi la Balochistan Liberation Army likikiri kutekeleza shambulizi hilo.
Hali ya hatari imetangazwa katika hospitali za mjini Quetta, wakati madaktari wakiagizwa kuwa katika zamu kushughulikia dharura hiyo.
Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amelaani shambulizi hilo kupitia ukarasa wake wa X.