Shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi yachochea uvumi wa uasi Burkina Faso

Martin Mwanje
1 Min Read
Kiongozi wa Junta, Kapteni Ibrahim Traoré, amekuwa mkimya tangu shambulio hilo kwenye kambi ya jeshi

Shambulizi ambalo limeripotiwa kuwauwa zaidi ya wanajeshi 100 kwenye kambi ya jeshi nchini Burkina Faso limezua uvumi kuhusu machafuko ndani ya vikosi vya usalama, katika nchi ambayo jeshi limekuwa madarakani tangu 2022.

Kiongozi wa kijeshi alionekana kwenye runinga ya serikali kukanusha uvumi huo.

Burkina Faso imekuwa ikipambana na waasi wa Kiislamu kwa miaka kadhaa na takriban nusu ya nchi hiyo iko nje ya udhibiti wa serikali.

Kundi la jihadi la Jamaat Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM) limesema ndilo lililohusika na shambulio la Jumanne iliyopita katika mji wa kaskazini wa Mansila.

Siku iliyofuata, kulikuwa na mlipuko karibu na makao makuu ya televisheni ya serikali.

Kulingana na ripoti kadhaa, watu wenye silaha walishambulia kambi ya kijeshi, iliyoko karibu na mpaka na Niger, tarehe 11 Juni.

Takriban wanajeshi 100 waliuawa na wengine wengi kutoweka, ripoti zinasema, na kuongeza kuwa mamia ya raia walikimbia Mansila kuelekea miji jirani kutafuta usalama.

Siku tano baada ya shambulio hilo kundi la JNIM, ambalo ni mshirika wa al-Qaeda, lilisema ndilo lililohusika na shambulio hilo, na kwamba makumi ya wanajeshi waliuawa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *