Shabana wailewesha Tusker, Homeboyz na Rangers watamba

Dismas Otuke
1 Min Read

Ligi Kuu ya Soka nchini Kenya imerejea leo huku Shabana FC wakiigutusha Tusker FC walipoizabua mabao 2-1 katika mechi iliyosakatwa katika uchanjaa wa Gusii.

Nahodha Charles Momanyi aliwaweka wageni kifua mbele kwa bao la dakika ya 11, kabla ya Shabana kurejea mchezoni kwa goli la dakika ya 45 lake Denis Okoth.

Zikisalia dakika 8 mechi ikamilike, Hezekiah Omuri aliunganisha pasi ya Austine Odongo na kuwapa Shabana ushindi muhimu.

Katika matokeo mengine, Posta Rangers imewalemea Nairobi City Stars 2-1 huku Kakamega Homeboyz ikiwabwaga Talanta FC bao moja bila jibu.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *