Shabana FC watoka nyuma na kuwateka nyara wanajeshi Ulinzi Stars

Dismas Otuke
1 Min Read

Shabana FC wametoka nyuma  na kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya wenyeji Ulinzi Stars, katikamchuano wa Ligi kuu uliosakatwa Jumapili alasiri katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex.

Stafod Odhiambo aliwaweka wenyeji kifua mbele kwa bao la dakika ya tano lakini Mathew Tegisi, akakomboa kwa wageni kutoka Kisii, katika dakika ya 45 na kipindi cha kwanza kuishia sare ya goli moja.

Tegisi aliwaweka  ‘Tore bobe’ uongozini kunako dakika ya 65, kabla ya Peter Glen kuwanusuru wenyeji kwa bao la dakika ya 5 ya ziada.

Kakamega Homeboyz pia walitoka nyuma mara mbili na kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya wagema mvinyo Tusker FC, huku Kariobangi  Sharks wakiwatia adabu Murang’a Seal mabao matatu bila.

Share This Article