Shabana FC wasaini mkataba wa udhamini wa shilingi milioni 20 na kampuni ya Bangbet

Dismas Otuke
4 Min Read

Mabingwa wa National Super League Shabana FC wamezindua kampuni ya Bangbet kuwa mfadhili rasmi kwa msimu wa ligi kuu wa mwaka 2023/2024 wa kima cha shilingi milioni 20.


Ushirikiano huo uliotiwa saini siku ya Jumapili katika kaunti ya Nairobi, utashuhudia Bangbet pia wakitoa jozi tatu ya sare za kuchezea na kufanyia mazoezi msimu wote kwa kila mchezaji.

Mlezi wa klabu hiyo Gavana wa kaunti ya , Kisii Paul Simba Arati, ametoa hahikisho kuwa ukarabati unaonendelea katika uwanja wa Gusii utakamilika hivi karibuni tayari kwa mechi za nyumbani na pia mazoezi ya timu hiyo .
“Kama mlezi wa klabu nawaomba viongozi wa jamii yetu na wale wanaopenda kuisaidia timu milango yetu i wazi njooni muongezee kila mko nacho kwa kile ambacho tayari tumepata tuachane na siasa ndogo,”akasema Arati

Arati amewataka viongozi wote wa eneo la Gusii kuinga mkono timu hiyo kuhakikisha wanasajili matokeo bora baada ya kupndishwa ngazi kufuatia Subira ya miaka 17.
“Imechukua muda mrefu kuishawishi Bangbet kuwekeza kwa timu yetu lakini nafurahia kuwa hatimaye wamekubaki na tumesaini mkataba naomba tusiwaangushe,”akaongeza Arati

Baadhi ya viongozi wamezungumzia kuhusu ukarabati unaoendelea katika uwanja wa Gusii ,na ningependa kutoa hakikisho kuwa kazi hiyo itakamilika kwa wakati ufaao kutumika kwa mechi za nyumbani na mazoezi ya timu msimu ujao.”akasisitiza Arati

“Nilivyoahidi awali udhamini wa shilingi milioni 20 kwa timu yetu ya shabana hatimaye umezaa matunda na vitu kama sare na mipira ya kuchezea pia imeshughulikiwa .

Ni ombi langu kwa wafdahili wengine na mashabiki kuiunga mkono katika majukumu yaliyo mbele na tuepuke siasa duni.”akatamatisha Arati

Mwenyekiti wa timu hiyo, Jared Nivaton,amefuchua kuwa tayari wamesajili wachezaji kadhaa katika harakati za kuimarisha kikosi tayari kwa msimu mpya wa ligi kuu utakaoanza Agosti 27.

“Tumesajili wachezaji kadhaa kuimarisha kikosi na tutawazindua hivi karibuni kabla ya kuanza kwa msimu .Tunaamini watatusaidia kuafikia malengo yetu ya kuwa miongoni mwa timu bora katika ligi kuu msimu wa mwaka 2023/2024 na kisha kutwaa ubingwa msimu wa mwaka 2024/2025 .”akasema Nivaton

“Pia ningependa kufafanua kuwa timu yetu in Patron mmoja ambaye ni gavana Paul Simba Arati na tunatakiwa kukamilisha majadala huo na kusonga mbele .Nawaomba mashabiki wetu na wote wanaotuunga mkono kuweka kando siasa kwenye timu yetu.”akaongeza
Afisa Mkuu Mtendaji wa Bangbet Leonardo Veresse amesema wataboresha udhamini huo baada ya msimu wa kwanza huku wakilenga kuhakikisha timu hiyo inasalia ligi kuu.

“Leo ni mwanzo wa safari yetu na Shabana ,na tunataka kuiboresha iwe timu kubwa.Ushirikiano wetu ni wa msimu mmoja kwa kiwango cha shilingi milioni 20 na Zaidi tutatoa jezi tatu za kuchezea,sare za mazoezi na mipira ya kuchezea.

Tutaongeza shilingi milioni 10 endapo timu hii itanyakua taji ya ligi kuu nchini.”akasisitiza Veresse

Sare za kuchezea  Nyumbani za Shabana FC msimu wa mwaka 2023/2024
Sare za kuchezea ugenini msimu wa mwaka 2023/2024

Shabana ambayo itakuwa timun ya tatu ya kijamii katika ligi kuu ya Kenya msimu wa mwaka 2023/2024 baada ya Gor Mahi ana AFC Leopardsitafungua msimu kwa kuchuana na Muranga Seal jijini Nairobi Agosti 27,kabla ya kucheza ugenini dhidi ya Talanta FC na kuwaalika Police FC katika mechi za pili na tatu mtawalia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *