SHA yatangaza malipo ya mwezi Oktoba kwa taasisi za afya

Maombi ya malipo yapatayo 217,700 yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 2.6 yalipokelewa kutoka kwa hospitali 2,382 mwezi Oktoba mwaka huu.

Marion Bosire
1 Min Read

Mamlaka inayosimamia bima mpya ya afya ya jamii SHA imetangaza malipo yaliyotolewa kwa taasisi mbali mbali za afya kwa huduma zilizotolewa mwezi Oktoba.

Kupitia taarifa iliyotiwa saini na kaimu afisa mkuu mtendaji Robert Ingasira, SHA imethibitisha kwamba zaidi ya bilioni 1.36 zimesambazwa na ni asilimia 52 ya malipo ya huduma zilizotolewa mwezi huo.

Maombi ya malipo yapatayo 217,700 yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 2.6 yalipokelewa kutoka kwa hospitali 2,382 mwezi Oktoba mwaka huu.

Kutokana na maombi hayo, maombi 53,554 yamelipwa kwa hospitali 1,195. Maombo 164,146 yaliyosalia ambayo ni jumla ya shilingi bilioni 1.2 yanashughulikiwa.

Yanapitia mchakato wa kuyathibitisha kwa lengo la kuhakikisha usahihi na uhalali wake.

SHA imetoa hakikisho kwamba malipo yaliyosalia ikiwa ni pamoja na ya mwezi Novemba, yatatolewa kufikia mwisho wa wiki ijayo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *