Sha Carri Richardson ndiye bingwa mpya wa dunia baada ya kuandikisha rekodi mpya jana Jumatatu usiku mjini Budapest nchini Hungary ya sekunde 10.65.
Bingwa mtetezi wa dunia katika mita 200 Shericka Jackson alinyakua nishani ya fedha huku Fraser Pryce akiridhika na shaba.
Ushindi wa Richardson aliye na umri wa miaka 23 ulizima ndoto ya Pryser ya kunyakua dhahabu ya 66 ya dunia katika mita 100.