Serikali yatoa shilingi milioni 550 kwa uboreshaji wa Shule za Alliance

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto siku ya Jumapili ametangaza kuwa serikali imetoa shilingi milioni 550 ,kugharamia ukarabati na uboreshaji wa shule za upili za Alliance kwa wavulana na wasichana zilizo katika kaunti ya Kiambu.

Ruto ametangaza haya siku ya Jumapili alipoongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 100 tangu kuasisiwa kwa shule ya upili ya wavulana ya Alliance.

Shilingi milioni 60 zitatumika kwa ujenzi wa madarasa mapya, nyingine 40 milioni zijenge academia ya michezo, na shilingi milioni 200 zitumike kwa ujenzi na ukarabati wa barabara karibu na shule hiyo.

Shilingi nyingine milioni 155 zitaelekezwa kwa ujenzi wa bweni la vitanda 640 katika shule jirani ya wasichana ya Alliance na kiwango kingine cha shilingi milioni 40 kikitengewa ujenzi wa madarasa 24.

Share This Article